Frank Mapunda: *NAPENDA KUFUGA KUKU*
SEHEMU YA NANE
Habari rafiki msomaji wa Makala hizi nzuri za ufugaji bora wa kuku, Leo nitakuwa na somo muhimu sana katika ufugaji wa kuku, nasema muhimu sana kwasababu usipozingatia katika hatua hii ni rahisi sana kupata hasara kubwa katika ufugaji wako Na kuona ufugaji wa kuku hauna faida na niwahasara sana, hivyo rafiki kama toka sehemu ya kwanza haukuwa makini kufatilia kwa makini masomo haya basi Leo weka umakini wako Mkubwa katika somo hili la leo,
UTUNZAJI WA VIFARANGA NA CHANJO MUHIMU KWA KUKU WAKO
Wafugaji wengi tunapoanza Kufuga huwa hatuna elimu sahihi juu ya ufugaji na kusababisha hasara kubwa sana katika ufugaji, changamoto kubwa inasababiswa na sisi wenyewe wafugaji kwa kutotafuta elimu sahihi ya ufugaji wa kuku, kubwa zaidi hata watu wanaotushauri ufugaji huu huwa hawatuambii kanuni bora za ufugaji na kinachufanyika ni kuangaika kutibu kuku baada ya kuingia magonjwa na hii inatusababishia hasara kwasababu vifo vingi Vya Vifaranga vinatokea, Mimi kipindi naanza ufugaji nilikuwa mmoja wa wahanga wa kupoteza kuku wengi kutokana na vifo hadi marafiki wangu wakaribu wakaniambia niachane na ufugaji huu unanitia umaskini hiyo yote kwasababu nilikosa elimu sahihi ya ufugaji wa kuku na baada ya kupata hasara kubwa nikakaa chini nikatafakari kwanini nimepata hasara hiyo nikatafuta maarifa kama mtu mwenye njaa anayetafuta chakula nilitembelea wafugaji wengi changamoto niliyoipata kwa wafugaji wengi wa Tanzania ni wabinafsi sana ila sikukata tamaa nikatafuta wataaramu wamifugo (siyo mmoja zaidi ya kumi) nikatafuta vitabu mbalimbali Vya ufugaji na baada ya kujifunza Vya kutosha nikapeleka elimu hii kwa vitendo nikapata matokeo mazuri sana sikupoteza kifaranga hata kimoja baada ya kunufaika nikaona nivyema nikushirikishe wewe rafiki yangu maarifa haya najuwa na ninauhakika yatakusaidia sana katika kufikia malengo yako ya ufugaji wakuku
✍UCHAGUZI BORA WA VIFARANGA
Rafiki ni muhimu sana kuwa mwangalifu katika kuchagua sehemu ya kununua Vifaranga, hakikisha sehemu unaponunua Vifaranga ni watu wanaozingatia chanjo sahihi kwa kuku wazazi hii itakusaidia sana kuepuka magonjwa ambayo Vifaranga watakuwa wamelithi kutoka kwa kuku wazazi ambayo itakusababishi vifo vingi Vya vifanga, kuku mzazi anatakiwa awe amepewa chanjo zote za magojwa na hii itasaidia Vifaranga vyako kuwa Na kinga ya kutosha
✍NYUMBA YA KULELEA VIFARANGA
Vifaranga wanahitaji uangalizi wa karibu sana kwasababu wanakuwa hawanauwezo wakujilinda na kujitafutia chakula hivyo wewe mfugaji unatakiwa uwe na chumba maalumu kwaajiri ya kuwatunzia Vifaranga wako chumba hicho kinatakiwa kiwe kimefanyiwa maandalizi yafuatayo
kama chumba chako ni chatofari basi hakikisha umekisafisha vizuri na ukutani uwe umwpaka chokaa, chokaa inasaidia kuua na kuepusha kuzaliana kwa bacteria mbalimbali ambao ni wasababishi wa magonjwa mbalimbali ya kuku,
Kama chumba chako ni cha mbao au marighafi nyingine ni muhimu ukafanya usafi na kwakutumia Dawa aina ya LAVENDER AU V-RID DISINFICTALIT, Dawa hii inasaidia sana kuuwa vimelea Vya magojwa
Ni muhimu mlango wa chumba cha kuku kuwe na dishi au kisima chenye maji na Dawa kati ya hizo nilizotaja hapo juu na kila utakapoingia kwenye banda lako lakuku lowesha kwanza miguu yako ili kuzuia bacteria/vimelea Vya magonjwa kuingia katika banda lako la kuku
kuna mabanda mbalimbali ya kulelea Vifaranga Vya kuku kama vile brunda au unaweza kutengeneza kwa mbao hata kugawa chumba chako kisehemu kidogo ili kuweza kutunza Vifaranga vyako,
pia unaweza kutumia mabox ambayo huwa yanakuja na pikipiki wanazotoka kununua (tembelea wanapouza pikipiki waulizie mabox watakuonyesha) mabox haya unayasafisha kwa Dawa niliyoeleza hapo juu na kutoboa sehemu ya kuwekea taa box moja linauwezo wakutunza Vifaranga 80-100
✍JOTO
Vifaranga vinahitaji joto kwasababu vinapokuwa vidogo havina uwezo wa kujikinga na baridi hivyo ni muhimu sana kuwa Na vyanzo Vya joto, vinaweza kuwa taa yenye uwezo wa kuzalisha joto nzuri, jiko la mkaa au Vyungu maalumu kwaajiri ya kutunzia joto ili kujuwa joto kama linakidhi Vifaranga utaona hali ya Vifaranga vyako kama ifuatavyo
VIFARANGA KULUNDIKANA
unapoona Vifaranga vimelundikana pamoja ujuwe joto lililopo halitoshi hivyo Vifaranga vinatafuta njia ya kukabiliana na joto na utakapoona hivyo ni muhimu ukawaongezea chanzo kingine cha joto
VIFARANGA KUKAA PEMBENI KABISA YA BANDA
Unapoona Vifaranga vyako vimekaa mbali na chanzo cha joto na havichangamki ujuwe joto lililopo ni kubwa hivyo punguza chanzo cha joto
VIFARANGA KUSAMBAA KATIKA BANDA HUKU WAKICHEZA NA KULA KWA FURAHA
Vifaranga vyako vinapopata joto sahihi na utaviona vinakula na kucheza kwa furaha hapo ujuwe joto lipo sawa
Vifaranga vinahitaji chanzo cha joto kwa mda wa majuma manne baada ya hapo havinatena na shida yakuwa na chanzo cha joto
✍MWANGA
Vifaranga vinahitaji mwanga ili visiweze kulaliana na kusababisha vifo kwa vifaranga
✍MAJI SAFI NA CHAKULA
Vifaranga vyako vinahitaji maji safi ya kunywa na chakula ili waweze kukuwa na kuwa Na Afya njema
✍RATIBA YA CHANJO MUHIMU KWA KUKU
Kuku wanahitaji chanjo ili kuwapa kinga katika miili yao ili kujikinga na magonjwa, iwapo mfugaji atashindwa kuzingatia chanzo hizo atapata hasara kubwa ya vifo Vya Vifaranga kwasababu kinga ni bora kuliko tiba, nimuhimu kwa mfugaji kuzingatia chanjo hizi ili kuwa na matokeo chanya katika mifugo yako
✍SIKU YA PILI HADI YA SITA
Siku hizi ni muhimu sana kuku wako kuwapa chanjo kwaajiri ya magonjwa ya matumbo pamoja na vitamini kwa kuwapa mifugo yako Dawa hizi utaepuka na vifo ambavyo vinatokea kwa Vifaranga
CHANJO
TRISULMYSINE+VITALYTE
iwapo utakosa (trisulmysine) unaweza kuwapa TRIMAZINE 30% AU COTRIM/TYPOPRIM kati ya hizo moja utatumia ukichanganya na vitalyte
dawa hii itasaidia kukinga kuku wako Na magojwa ya matumbo
✍SIKU YA 7
utawapa chanjo ya kideli
Hii unachanganya na maji unawapa wanakunywa
MUHIMU; Dawa hii inatumika kwa mda wa masaa mawili tu na siyo zaidi iwapo utazidisha itageuka kuwa sumu na kuleta Athali kwa mifugo yako
DAWA
NEWCASTLE
✍ SIKU 8-13
Kama utaona kuku wako wanaonyesha dalili ya kuzubaa ni utarudia kuwapa Dawa ambazo uliwapa siku ya 2-6
✍SIKU YA 14
Utawapa chanjo kwaajiri ya gumburo
✍SIKU YA 16-18
utawapa kuku wako chanjo kwaajiri ya magonjwa ya kipindupindu cha kuku (fowl cholera), ugonjwa wa matumbo (fowl typhoid)
DAWA
Esb3 30%
✍SIKU YA 21
Rudia kuwapa kuku wako chanjo ya kidele (Newcastle)
✍SIKU YA 22-27
wape vitalyte; hii ni kwaaji ya kuongeza vitamin I mwilini
✍SIKU YA 28
ludia kuwapa chanjo ya gumburo
✍HADI KUFIKIA HAPO UTAKUWA UMEOKOA KWA KIASI KIKUBWA KUKU WAKO KATIKA HATARI YA VIFO NA MAGONJWA MBALIMBALI YA MIFUGO YAKO (BADO TUNAENDELEA)
✍MIEZI 2
CHANJO YA NDUI
Hii huwa wanachoma sindano kwenye mabawa
✍MIEZI 2 WIKI YA KWANZA
Wape OXTETRACYCINE 20%(OTC 20%)+VITALYTE
Hii itasaidia kuku wako kujikinga na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya bacteria
✍MWEZI WA 2 WIKI YA 2
wape kinga kwaajiri ya minyoo, na matumbo
DAWA
GENTAMYCINE SULPHATE (Hii ni yasindano), au TYPOPRIME AU ESb3 30%, au TRIMAZINE 30%, au SULFONAMIDE
kama utatumia sindano wachomwe 0.5mls,
✍MWEZI WA TATU
Utarudia kuwa NEWCASTLE
✍MWEZI WA NNE
Utawapa kuku wako chanjo kwaajiri ya magojwa ya kipindupindu cha kuku pamoja na matumbo
DAWA
OXTETRACYLIN 20% (OTC 20%)+VITALYTE KAMA UTAKOSA HIYO UTAWAPA KATI YA HIZI MOJA; AMINTOTA/VITASTRES/ANT-STRESS/
✍HADI KUFIKIA HAPO UTAKUWA UMEFIKIA MWISHO WA CHANJO MUHIMU KWA MIFUGO YAKO ZAIDI UTAKUWA UNARUDIA DAWA CHANJO YA KIDELI KILA BAADA YA MIEZI MITATU
kwa leo naomba niishie hapa tutakutana tena kesho Mungu akitujaria uzima
Makala Hii imeletwa kwako nami
FRANK MAPUNDA,
Kwa mahitaji ya Vifaranga aina ya KROILA karibu vinapatikana Vifaranga vyenye ubora na Afya njema kwasababu kuku wazazi walipewa chanjo zote za magonjwa,
Pia kwamahitaji ya Mayai kwaajiri ya kutotoresha yanapatikana,
Pia kwa mahitaji ya MASHINE kwaajiri ya kutotoresha (incubator) zinapatikana zipo za aina zote mafuta ya taa na zaumeme
Nikutakie siku njema na ufugaji wenye mafanikio
Endelea kunifatilia.............!
[12/18, 07:11] Frank Mapunda: *NAPENDA KUFUGA KUKU*
SEHEMU YA TISA
Habari rafiki msomaji wa Makala hizi za Napenda Kufuga kuku, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na mapambano ya maisha hongera sana, leo nimependa nizungumze na wewe mambo mazuri kuhusu ufugaji wa kuku natumaini hadi kufikia hapa kuna mambo mengi utakuwa umejifunza ambayo yataenda kukusaidia wewe katika ufugaji wako wa kuku
UKATAJI MIDOMO WA KUKU
Ni jambo la muhimu sana kwa kuku kukata midomo na hii huwa inasaidia kukuwako wasiweze kula Mayai na tabia nyingine mbaya ya kudonyoana, kuku wanatakiwa wakatwe midomo katika wiki ya kumi na nane hadi kumi na tisa ,iwapo kuku wako wameanza mapema tabia mbaya ya kudonyoana unaweza ukawakata mapema zaidi kuanzi wiki ya kumi na tano na kuendelea
SABABU YA KUKU KUDONYOANA
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinachangia kuku kuwa na Tabia mbaya ya kudonyoana hapa nitazitaja baadhi ya sababu
kuku kuwa na mlundikano mkubwa katika banda moja;
Hii inachangia sana kuku kuwa na tabia mbaya ya kudonyoana kwasababu kuku wanakuwa na mlundikano mkubwa ambao unawasababishia wakose shughuri nyingi za kufanya
Vyombo vichache Vya chakula na maji
Upungufu wa madini na vitamin;
Kuku anapokosa madini mbalimbali mwilini anajisikia raha kumdonyoa mwenzake
Mwanga mkali kupita kiasi
JINSI YA KUDHIBITI TABIA MBAYA YA KUKU KUDONYOANA
Ni muhimu kuku wako wakapewa majani kama vile chainize, mchicha, kabeji, azolla, hydronic fodder itasaidia kwa kiasi kikubwa san a kuku wako kuacha kabisa na tabia ya mbaya ya kudonyoana
wapewe Dawa ya vitamini kwa wingi kama vile EGMYCINE,MULTIVAMIN, AMIN TOTAR, VITALYTE
Wawekee bembea; bembea itasaidia kuku wako wawe na shughuri nyingi za kufanya ambazo zitasaidia kuku kusahau tabia mbaya ya kudonoana
wasilundikane wengi kwenye eneo Dogo
MADHARA YATAKAYOSABABISHWA NA KUKU KUDONOANA
Kama utashindwa kuwadhibiti mapema kuku wengi watakufa hivyo kupata hasara
Kuku wanaotaga watasimama kutaga kutokoana na mstuko wa vidonda vilivyosababishwa na kudonoana
✍Iwapo utazingatia maelezo ya hapo juu utaweza kuwazuia kwa kiasi kikubwa kuku wako kudonoana
kuku wako watakuwa vizuri na wakupendeza
hasara ya vifo haitakuwepo tena
LISHE BORA YA KUKU
Ili kuku wako waweze kuwa na Afya njema ni muhimu sana ukazingati lisho bora ya kuku ili iweze kunufaika na ufugaji wako, kuku wanahitaji chukula chenye virutubisho vyote Muhimu, kama vile
Chukula cha kutia nguvu
kujenga mwili
kulinda mwili
Kuimarisha mifupa
wanahitaji maji safi,
VYAKULA VYA KUTIA NGUVU
Hivi ni vyakula muhimu sana kwa kuku na iwapo kuku hatakosa vyakula hivi kuku wako hawataweza kukua vizuri baadhi ya vyakula Vya kutia nguvu ni kama ifuatavyo
Pumba za mahindi,
pumba laini za mpunga,
pumba za ngano,
cheng za mahindi
chenga za mchele,
mtama
uwele
ulezi
Magimbo
Mihigo
viazi vitamu
Hydroponics fodder
Azolla
VYAKULA VYA KUJENGA MWILI
vyakula hivi vinaumuhimu sana kwa kuku wako ndivyo vinavyohusika na ukuaji mzima wa kuku, ni muhimu sana kuwapa kuku wako chakula hiki, hivi ni baadhi vyakula Vya kujenga mwili
Mashudu
Alizeti
mawese
karanga
Soya
korosho
Ufuta
Damu ya wanyama iliyokaushwa
minyoo,
mayai ya wadudu
Mchwa
wadudu
Funza
Hydroponic fodder
Azalla
KUIMARISHA MIFUPA
Hili pia ni kundi la vyakula muhimu sana kwa kuku wako, vipo Vya vingi Mimi nitataja tu baadhi yake
Maganda ya Mayai yaliyosagwa vizuri
madini ya chokaa(Calcium), (phosphorus), maganda ya konokono
majivu ya mifupa iliyosagwa vizuri
Chumvi ya jikono
Hydrophobic fodder
Azolla
VYAKULA VYA KULINDA MWILI
Hivi nivyakula muhimu sana kwa kuku wako, vipo vingi hapa nitataja tu baadhi yake
Mboga mboga
mchwa,
Samadi ya ng'ombe mbichi ambayo haijakaa mda mrefu,
Mchicha pori
chaines
kabeji
mchanganyiko wa vitamin vilivyotengenezwa viwandani (Vitamin primix)
juwa la Asubuhi na jion linavitamini A na D
Hydropnic fodder
Azolla
NJIA ZA KUCHANGANYA VYAKUKA VYA KUKU
Zipo njia kuu mbili ambazo unaweza kutumia kuchanganya chakula cha kuku
MASHINE
Hii hutumika mala nyingi viwandani au kwa wafugaji wakubwa
MAJUMBANI (Njia ya mikono)
Hii ndio njia ambayo utumika na wafugaji wengi
VIFAA MUHIMU VYA KUCHANGANYIA CHAKULA MAJUMBANI
KOLEO (SPEDE)
VIINI LISHE
VIROBA AU MAGUNIA
TURUBA/SAKAFU SAFI
JINSI YA KUCHANGANYA CHAKULA
1)VYAKULA VYA MADINI
Chokaa, Chumvi na mifupa
2)DDamu na unga wa samaki au dagaa
3)Mashudu ukichanganya na mchanganyiko wakwanza na wapili
4)Pumba utachanganya na mchanganyiko wa tatu
✍kuna njia mbili ambazo MTU unaweza kutumia ili kupata mchanganyiko sahihi
KUNUNUA CHAKULA AMBACHO TAYARI KIMESHA CHANGANYWA
KUCHANGANYA WEWE MWENYEWE
✍ILI UWEZE KUWA NA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU NI LAZIMA UANDAE WEWE MWWNYEWE NYUMBANI
✍KWAKUTENGENEZA CHAKULA WEWE MWENYEWE NYUMBANI UTAWEZA KUPUNGUZA GHARAMA KWA ASILIMIA KUBWA KULIKO UKINUNUA CHAKULAQ KILICHO CHANGANYWA KABISA
NAOMBA NIISHIE HAPA KWA SASA BAADAE NITAKUJA TENA NA UWIANO WA MICHANGANYIKO YA CHAKULA CHA KUKU AMBACHO UTAWEZA KUTENGENEZA WEWE MWENYEWE NYUMBANI HIVYO USIPANGE KUKOSA SOMO HILO
Ni Mimi rafiki yako
FRANK MAPUNDA
Kwa huduma na msaada zaidi tunaweza kuwasiliana moja kwa moja nami kwa namba
0758918243/0656918243
kwa mahitaji ya Vifaranga aina ya KROILA vinapatikana karibu nikuhudumie
Pia kwa mahitaji ya Mayai kwaajiri ya kutotolesha Vifaranga karibu sana yanapitikana,
Pia kwa mahitaji ya MASHINE KWAAJIRI YA KOTOTORESHA (INCUBATOR) ZINAPATIKANA ZIPO ZA MAFUTA YA TAA NA ZAUMEME
HUDUMA ZOTE ZINAPATIKANA POPOTE PALE ULIPO WOTE MNAKARIBISHWA
Endelea kunifatilia...............!
[12/20, 14:23] Frank Mapunda: *NAPENDA KUFUGA KUKU*
SEHEMU YA KUMI
Habari Rafiki msomaji wa makala za ufugaji wa kuku karibu sana katika somo letu la leo, leo tunaenda kujifunza jinsi ya kuandaa michanganyiko ya chakula cha kuku pamoja kiasi cha chakula kinachohitajika kwa kuku kingana na umri,
KWANINI TUJIFUNZE MICHANGANYIKO YA CHAKULA NA SIYO KWENDA KUNUNUA CHAKULA KILICHOCHANGANYA KABISA
Najuwa unaweza kujiuliza swali hilo lakini lengo KUU za Makala hizi za "Napenda Kufuga kuku" ni kukupatia maarifa yote sahihi kuhusu ufugaji wa kuku na jinsi ya kupunguza gharama za ufugaji bila kipunguza ubora wa mifugo yako, sababu kubwa ya kujifunza jinsi ya kuandaa michanganyiko ya chakula ni sisi wafugaji kuwa na elimu sahihi ya ufugaji na utengenezaji wa chakula nyumbani,
FAIDA ZA KUCHANGANYA CHAKULA SISI WENYEWE;
Kunafaida nyingi sana lakini hapa nitataja baadhi ya faida ambazo wewe mfugaji utazipata
UTAPUNGUZA GHARAMA YA CHAKULA
Iwapo wewe mfugaji utatengengeneza chakula wewe mwenyewe utapunguza kwa asilimia kubwa gharama za chakula kwasababu gharama zakununua michanganyiko na kuchanganya ni ndogo kuliko gharama ya kununua chakula dukani
UTATENGENEZA CHAKULA CHENYE UBORA
Iwapo utatengeneza chakula wewe mwenyewe utatazingatia vitu muhimu vyote na utaweka kwa ubora unaotakiwa
KWANINI NAPENDEKEZA SANA UTENGENEZE CHAKULA WEWE MWENYEWE
Baadhi ya watu wanaotengeneza chakula wanatengeneza chini ya kiwango na hii inaenda kumwasili moja kwa moja mfugaji wa kuku kwa kuku wake kupata magonjwa ya lishe na kushindwa kukuwa vizuri kwasababu ya lishe isiyokuwa na viwango,
Ngoja nikupe habari moja kutoka kwangu mwenyewe "mwanzo kipindi naanza ufugaji wa kuku nilikutana na changamoto kuku wangu kuugua mala kwa mala magojwa ya lishe nilipokaa chini na kutafakari huku nikishauliana na mtaalamu wa mifugo ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo tukaja na majibu yasiyo ya uhakika ya kufanya majaribio ya kubadilisha mfumo wa chakula kutoka kununua chakula moja kwa moja hadi kuja kuchanganya sisi wenyewe baada ya kufanya jalibio hilo tukaja kugundua kwakutengeneza chakula sisi wenyewe kuku hawakupatwa tena na changamoto ya magonjwa ya lishe toka hapo tukaja na maazimio ya kutokununua chakula moja kwa moja Bali tutakuwa tunatengeneza wenyewe na kwa kutengeneza wenyewe tukaja kuona tunapunguza gharama kwa kiasi kikubwa"
Leo sita kuwa na mambo mengi kuhusu chakula cha KUKU kwasababu katika SEHEMU YA TISA tulielezana kwa undani makundi ya chakula leo nitaenda kukupa michanganyiko ya chakula kuanzia siku sifuri hadi utakapoamua kusema basi kwa ufugaji wako, nitaeleza aina za michanganyiko utakayoenda kununua dukani (duka la mifugo) na idadi ya pumba utakayochanganya,
AINA ZA CHAKULA CHA KUKU(chakula hili ni chakuku wa Mayai,chotara na kienyeji tu na siyo KUKU wa nyama)
Kuna makundi matatu ya chakula makundi haya yanatofautiana na umri wa KUKU
1) wiki 0 hadi wiki 8
Kinaitwa SUPER MASH
2)Wiki 9 hadi 15
GROWER MASH
3)Wiki 16 nakuendelea
LAYERS MASH
✍MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU KUANZIA SIKU MOJA HADI WIKI NANE
*MUHIMU* KATIKA MICHANGANYIKO YOTE TUNACHONUNUA DUKANI NI MICHANGANYIKO TU NA TUNACHANGANYA NYUMBANI WENYEWE K
NA PUMBA HIVYO NITATAJA IDADI YA DEBE ZA PUMBA UTAKAZOTUMIA KUCHANGANYA MICHANGANYIKO YAKO NITAELEZA MICHANGANYIKO KUANZIA DEBE KUMI NA MBILI HADI DEBE MBILI
SEHEMU YA KWANZA UMRI WA WIKI O-8
CHAKULA.
PUMBA DEBE 12
MASHUDU KILO 30
DAGAA KILO 12
CHOKAA. KILO 6
DAMU KILO. 2
VIGOSTART. KILO 1
DCP. KILO 1
PREMIX KILO 1
MIFUPA KILO 1
CHUMVI NUSU KILO
MICHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU WA WIKI O-8
CHAKULA.
PUMBA DEBE 10
MASHUDU KILO 25
DAGAA KILO. 10
CHOKAA KILO 4
DAMU KILO. 2
VIGOSTART KILO 1
DCP. NUSU KILO
PREMIX NUSU KILO
MIFUPA. KILO 1
CHUMVI NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU WA WIKI 0-8
CHAKULA
PUMBA DEBE 6
MASHUDU KILO 20
DAGAA. KILO 8
CHOKAA. KILO 2
DAMU KILO 2
VIGOSTART. KILO 1
DCP. KILO 1
PREMIX. NUSU KILO
MIFUPA KILO 1
CHUMVI NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU KWA WIKI 0-8
CHAKULA
PUMBA DEBE 4
MASHUDU. KILO 12
DAGAA KILO 5
CHOKAA KILO 1
DAMU. KILO 1
DCP. ROBO KILO
PREMIX. ROBO KILO
MIFUPA. NUSU KILO
CHUMVI. ROBO KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU KWA MDA WA WIKI 0-8
CHAKULA
PUMBA DEBE 2
MASHUDU. KILO 6
DAGAA. KILO 3
DAMU. NUSU KILO
DCP ROBO KILO
PREMIX. ROBO KILO
MIFUPA. NUSU KILO
CHUMVI. ROBO KILO
SEHEMU YA PILI UMRI WA WIKI 9- 16
CHAKULA
PUMBA DEBE 12
MASHUDU KILO 30
DAGAA KILO 12
CHOKAA KILO 8
DAMU. KILO 3
DCP. KILO 1
PREMIX. KILO 1
MIFUPA. KILO 2
CHUMVI. KILO 1
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
CHAKULA
PUMBA DEBE 10
MASHUDU KILO 25
DAGAA. KILO 8
CHOKAA. KILO 6
DAMU. KILO 2
DCP. NUSU KILO
PREMIX. NUSU KILO
MIFUPA. KILO 1
CHUMVI. NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
PUMBA DEBE 6
MASHUDU KILO 18
DAGAA KILO 6
CHOKAA. KILO 4
DAMU. KILO 2
DCP. NUSU KILO
PREMIX. NUSU KILO
MIFUPA. KILO 1
CHUMVI NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA.
CHAKULA
PUMBA DEBE 4
MASHUDU. KILO 9
DAGAA KILO 3
CHOKAA. KILO 2
DAMU. KILO 2
DCP. ROBO KILO
PREMIX. ROBO KILO
MIFUPA. ROBO KILO
CHUMVI. ROBO KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
CHAKULA
PUMBA DEBE 2
MASHUDU KILO 6
DAGAA. KILO 2
CHOKAA. KILO 1
DAMU. ROBO KILO
DCP. ROBO KILO
PREMIX ROBO KILO
MIFUPA. ROBO KILO
CHUMVI. ROBO KILO
SEHEMU YA TATU UMRI WA WIKI 17 NAKUENDELEA
CHAKULA
PUMBA DEBE 12
MASHUDU KILO 30
DAGAA KILO 12
CHOKAA. KILO 12
DAMU. KILO 3
GLP. KILO 1
PREMIX. NUSU KILO
MIFUPA. KILO 1
CHUMVI. NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
CHUKULA
PUMBA DEBE 10
MASHUDU KILO 25
DAGAA. KILO 10
CHOKAA. KILO 10
DAMU. KILO 2
GLP. KILO 1
PREMIX. NUSU KILO
MIFUPA. KILO 1
CHUMVI. NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
CHAKULA
PUMBA DEBE 6
MASHUDU. KILO 20
DADAA KILO 8
CHOKAA. 7
DAMU. KILO 2
GLP. KILO 1
PREMIX. NUSU KILO
MIFUPA. KILO 1
CHUMVI. NUSU KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
CHAKULA
PUMBA DEBE 4
MASHUDU KILO 10
DAGAA KILO 4
DAMU. KILO 2
GLP KILO 1
PREMIX. ROBO KILO
MIFUPA. NUSU KILO
CHUMVI. ROBO KILO
MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA KUKU
CHAKULA
PUMBA DEBE 2
MASHUDU KILO 6
DAGAA KILO 2
CHOKAA. KILO 2
DAMU. KILO 1(
GLP NUSU KILO
PREMIX. ROBO KILO
MIFUPA. NUSU KILO
CHUMVI. ROBO KILO
Huo ndio mchanganyiko wa chakula cha kuku nenda duka la mifugo utapata michanganyiko hiyo yote
KIASI CHA CHAKULA AMBACHO KUKU WANAKULA KWA MDA WA WIKI SIFURI NAKUENDELEA
1WIKI GRAM 12
2WIKI GRAM 22
3WIKI GRAM 27
4WIKI GRAM 32
5WIKI GRAM 38
6WIKI GRAM 42
7WIKI GRAM 46
8WIKI GRAM 50
CHAKULA KINACHOHITAJIKA NI SUPER STARTER
CHAKULA CHA KUKU KUANZIA WIKI 9-16
KINAITWA GROWER MASH
9 WIKI GRAM 56
10 WIKI GRAM 62
11 WIKI GRAM 64
12 WIKI GRAM 66
13 WIKI GRAM 68
14 WIKI GRAM 74
15 WIKI GRAM 76
16 WIKI GRAM 80
CHAKULA CHA KUKU KUANZIA WIKI YA 17 NAKUENDELEA
CHAKULA TUNAKIITA LAYERS MASH
17 WIKI GRAM 82
18 WIKI GRAM 88
19 WIKI GRAM 92
20 WIKI GRAM 102
21 WIKI GRAM 108
22 WIKI GRAM 110
23 WIKI GRAM 116
24 NA KUENDELEA GRAM 120
MUHIMU KUZINGATIA LISHE BORA KWA MATOKOEA BORA YA MIFUGO YAKO, JAMBO LA MUHIMU NA LAKUZINGATIA NI KUWA NA VYOMBO AMBAVYO HAVITASABABISHA UPOTEVU MKUBWA WA CHAKULA ,
KUKU WANATABIA YA KUPALUA PALUA HIVYO UKIWEKA KWENYE VYOMBO AMBAVYO KUKU NI RAHISI KUMWAGA UTAPATA HASARA YA CHAKULA NI MUHIMU KUWA NA VYOMBO BORA
Najuwa mwanzo wa Makala hizi nilizungumzia kuhusu kutatua changamoto ya magonjwa ambayo imekuwa ikiwasumbua wengi, kuna watu wanajiuliza mbona hakuna sehemu niliyoeleza msijali ipo kwenye mfululizo wa masomo yetu ya mbele na somo hilo lipo katika SEHEMU YA KUMI NA SABA, pia nilieleza kuhusu mbinu/kanuni ya kupunguza gharama ya chakula cha kuku hadi Asilimia Hamsini nalo msijili somo hilo lipo katika mfululozo wa Makala zetu na lipo SEHEMU YA KUMI NA NANE, KUMI NA TISA NA SEHEMU YA ISHIRINI
Hivyo msijali natumaini baada ya kumaliza mfululizo wa Makala hizi tutakuwa na Elimu ya kutosha katika ufugaji wa kuku
Makala hii imeletwa kwako namimi
FRANK MAPUNDA,
KWA MAHITAJI YA VIFARANGA CHOTARA AINA YA KROILA VINAPATIKANA KARIBU TUKUHUDUMIE,
PIA KWA MAHITAJI YA MAYAI KWA AJIRI YA KUTOTORESHA MAYAI YA KUKU CHOTARA AINA YA KROILA KARIBU SANA YANAPATIKANA,
PIA KWA MAHITAJI YA MASHINE YA KUTOTORESHEA VIFARANGA ZINAPATIKANA ZIPO ZA AINA ZOTE ZA MAFUTA YA TAA NA ZAKUTUMIA UMEME KARIBU TUKUHUDUMIE, KWA MAWASILIANO ZAIDI
TUWASILIANE KWA NAMBA
0758918243/0656918243
FURAHA YANGU NIKUONA WEWE RAFIKI UNAFANIKIWA KATIKA UFUGAJI WAKO
Endelea kunifatilia............!
|
MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani. Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...
Comments
Post a Comment