MWANDISHI, AMINA SANGA.
Moja kati ya kosa ambalo watu wengi wanafanya/ walishawahi kuyafanya ni kutaka KUELEWEKA. Wengi wetu tumejikuta tunachelewa kufanya / kutimiza ndoto, mipango, vitu tunavyovitamani kwasababu ya kutaka kueleweka. Unataka kila mtu akuelewe Kwamba una mipango mikubwa, Kila mtu a appreciate, halafu inakuja kuwa kinyume na hivyo na unaishia kukata tamaa, kwasababu unataka tu ueleweke.
IPO HIVI, binadamu wengi huwa hawaelewi MCHAKATO. , ukiwa kwenye mchakato si rahisi watu kukuelewa, watu wanaelewa zaidi MATOKEO, na si ajabu yuleyule aliyekukatisha Tamaa akawa wa Kwanza kushangilia MATOKEO.
Lakini pia, sio kila unachokifanya watu wajue( keep them under low profile) Kwa usalama wako. Don't post everything, don't speak everything. Don't let them predict your future. Ukitaka kueleweka utajikuta unaishia hapohapo ulipo. Work hard in silence let success make noise (quoted)
Usimuamini kila mtu, usimuweke karibu kila mtu. Kuna vitu kaa navyo mwenyewe mpaka vitokee, wengine wangeshakua wamefanya vitu vikubwa, wengine wangekua wameandika vitabu vingi, hawachukui hatua kwasababu wanataka kueleweka. Usilazimishe watu wakuelewe, sio lazima. WE PAMBANA, You're the captain of your own ship.
Amina Sanga
Nguvu ya Uthubutu
Amina Sanga
Nguvu ya Uthubutu
HAKIKA AMINA UMENIFUNDISHA KITU MUHIMU, NIKO DARASANI KUJITAFAKARI KWA MANENO HAYO HAPO JUU, NAHISI ITANICHUKUA MUDA ZAIDI KUURUDIA HUU UJUMBE MPAKA NIELEWE VIZURI KWA FAIDA YANGU NA YA WENGINE PIA
ReplyDelete