https://yopocodetanzania.blogspot.com
NAMNA
YA KUENDESHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI
POWERED BY YOPOCODE TANZANIA
Vijana wenzangu popote mlipo Tanzania na duniani kote,poleni kwa mahangaiko ya kuendelea kutafuta mkate na kutafuta njia
ya kufafikai mafanikio makubwa kiuchumi na kimaendeleo. katika maandiko ya vitabu vya dini imeandikwa
asiyefanya kazi na asile,na mwanaume atatafuta kwa jasho na mwanamke atazaa kwa
uchungu,hii yote ni kudhihilisha
kuwa ni lazima kila mtu afanye kazi kulingana na kipawa alichojaaaliwa na
mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na vyote vilivyopo katika uso wa duniani.
Najua kila kijana ana namna anavyotafuta Ridhiki yake ilimradi tu inakuwa
halali, wapo wanaofanya kazi mmoja mmoja, wapo walioajiriwa serikalina, taasisi
za serikali,
taasisi na mashirika binafsi, lakini wapo ambao
wameamua kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali za kijasiariamali, wapo wakulima, wafanyabiashara, mmoja na hata walioamua kuunda vikundi ili kuona
namna gani nguvu ya pamoja inaweza kuwafikisha pale wanapotaka kufika, yote kwa yote mkono unaingia kinywani.
Leo ni
fursa kwa wale ambao wameamua kuwa katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali
na biashara, kuweka na kukopa n.k kwani
watajifunza mengi kupitia Kitabu hiki cha dira ya
kijana Tanzania.
Maana ya neno kikundi ni?
Kikundi ni mkusanyiko wa watu kadhaa wenye rika linalofanana au kutofautiana, yaweza kuwa jinsia moja au tofauti ambao wameamua kufanya shughuli za kujiingizia kipato kwa
mujibu wa sheria
pamoja na kujadili mambo
mbalimbali yanayohusu maendeleo yao.
Nitajikita zaidi katika
kujadili kuhusu vikundi vya vijana
wenye umri kati ya miaka 15-35, hili ni rika ambalo linachangamoto nyingi sana za
kimaisha katika jamii yetu.
NAMNA
YA KUUNDA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI KWA VIJANA
Hatua
ya kwanza
Ni lazima mtafute vijana kwanza ambao mnalengo la
kuunda kikundi chenu
yaani vijana mnaofahamiana kitabia, wenye nidhamu na heshima katika kazi, wenye
tabia njema kwa jamii inyowazunguka, vijana msio na tabia ya wizi, ubakaji,
ulevi na utumiaji madawa ya kulevya, vijana wenye uthubutu na bidii katika
kazi.
Kwa kukosa sifa
zinazoendane hapo ndipo vijana wengi
huwa tunashindwa na kujikuta baada ya miezi miwili kikundi kimekufa. Ni vizuri tukaanza kwa kutambuana kwanza, sisi wenyewe kuwa ni vijana wa aina gani,tunataka kujiunga kwa sababu gani,je sababu tu ni
kelele za viongozi kuwa tujiunge kwenye vikundi?.Eneo hili linahitaji
fikra na busara sana, mkishindwa
hapa huko mbele hakuna litakalofanyika.
Hatua
ya pili
Ni muhimu kikundi kikawa na malengo ya muda mafupi na malengo ya muda mrefu ambayo yamepangwa pamoja na wanakikundi wenyewe
siyo mtu mmoja apange kwa niaba ya watu wengine, malengo hayo yaweza kuwa ya miezi mitatu, miezi
sita, mwaka na hata miaka mitano kulingana na aina ya
shughuli mtakazokuwa mnafanya.
Malengo yakipangwa na wanakikundi wote inakua
raisi kutekelezeka kwani kila mtu anaona yeye ni familia ya kikundi kile, lakini mkishindwa kuwa na ushirikiano basi ni
vigumu kuyafikia malengo yenu.
Hatua
ya tatu
Ni muhimu kutafuta uongozi wa muda kwani hapa ndiyo mahali ambapo
uongozi wa muda unatafutwa ili uweze kuratibu na kusimamia shughuli za
kuimarisha kikundi,
najuwa mpaka kufikia hatua hii kikundi bado kinakuwa kinapitia changamoto nyingi sana wapo watakaoona
wanapoteza muda,
wapo watakaokua wanajaribu tu
kama mtaweza fika mbali n.k
Hatua
ya nne
Kuandaa mchakato wa utengenezaji wa katiba ya
kikundi,
hapa ndipo jina la kikundi
hupatikana,
malengo na shughuli zitakazofanywa
na kikundi hujadiliwa na kwa kina, majukumu
ya viongozi watakaochaguliwa yatakua ni yapi, adhabu na mafao ya mwanakikundi, kwa kifupi katiba ndiyo
mhimili wa kikundi,
ikikosewa hapa ndio dira na
muelekeo wa kikundi utakuwa
unaenda kombo.
Katiba ni lazima ijadiliwe na
wanakikundi wote.
Hatua
ya tano
Ni kusajili kikundi cha ujasiriamali cha
vijana. Ili kuweza kusajili kikundi cha vijana panahitajika kuwepo kwa
katiba.baada ya katiba kuwa tayari itwasilishwa
halmashauri kuomba usajili.
NAMNA
YA KUENDESHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI VYA
VIJANA
i) Kutengeneza katiba iliyobora.Kikundi ni lazima
kitengeneze katiba ambayo itatoa muongozo wa namna ya kujiendesha, majukumu ya viongozi na wajumbe wengine wa
kikundi.
Katiba ya kikundi ni lazima
ipendekezwe na wajumbe wengine ili kila kitu kilichomo kwenye katiba kieleweke
na kila mjumbe.
Sio vizuri na ni mbaya kunakili
katiba ya watu wengine na kuifanya iwe yenu kwani vikundi hutofautiana kwa aina
ya watu waliopo na shughuli wanazofanya.
ii) Kuwa na uongozi imara.Kikundi ni lazima kiwe na
uongozi imara katika kusimamia shughuli mbalimbali za uzalishaji na utawala.Ni
muhimu kuchagua viongozi wenye nia na lengo la kufanikisha kikundi kinasonga
mbele,usimchague mtu sababu/kiongozi sababu ni ndugu au rafiki yako au
mnafahamiana.
iii) Wanakikundi lazima waheshimiane wao wenyewe bila
ubaguzi wa aina yoyote ile wa rangi,jinsia,kitikadi,kiuchumi,kuwa na nidhamu ya
matumizi ya pesa na mali zingine za kikundi.
iv) Ni lazima maamuzi yanayofanywa ndani ya kikundi
yafuate sera,sheria na kanuni zilizowekwa na kupitishwa na wanakikundi wenyewe.Maamuzi
yasifanyike kwa kumkandamiza mtu au kikundi cha watu Fulani ndani ya kikundi.
v) Kikundi pia lazima kiwe na mikakati ya kubuni
miradi ya uzalishaji mali ambayo ina tija kwa wanachama wake,miradi hiyo yaweza
kubuniwa na wanachama wenyewe au kuomba msaada toka kwa wadau wengine wa
serikali na mashirika binafsi.Vile vile kikundi lazima kijenge utamaduni wa
kuaminiana baina ya viongozi na wanachama wenyewe,kwani hii huongeza mahusiano
mazuri baina ya wanachama na kupelekea kikundi kufanikiwa.
vi) Viongozi wa kikundi lazima muwe na utaratibu wa
kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya kikundi,ni muhimu kutafuta
taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya vijana na stadi mbalimbali za maisha
ili muweze kujiendesha kiuchumi na kijamii pia.Kila mwanakikundi awe kiongozi
na asiwe kiongozi ni lazima ayaweke maslai ya kikundi mbele kuliko maslai
binafsi,ni vibaya kutumia pesa na mali za kikundi kwa kujinufaisha mwenyewe.
vii) Viongozi wa kikundi wanajukumu la kuhakikisha
kunakuwa na mgawanyo mzuri wa majukumu kwa wanakikundi na
wafanyakazi walioajiriwa ili shughuli zote za kikundi ziweze kwenda kama
zilivyopangwa.
viii) Vilevile wanakikundi wanatakiwa kuwa na mtazamo wa
mbali na kuweka mawazo yao katika mpangilio mzuri wa kutekelezeka.
ix) Ni muhimu pia kuwa na vikao vya ndani vilivyowekwa
kwa mujibu wa sheria na katiba ya kikundi. Kutofanya vikao kunaweza kuibua maneno baina ya wanakikundi na
kukigawa kikundi.
Pamoja
na hayo yote,vikundi vingi vya ujasiriamali vya vijana vinakumbwa na changamoto
nyingi sana na hivyo kushindwa kuyafikia malengo kama ifuatavyo:
Vijana wengi waliopo kwenye vikundi vya
ujasiriamali wana haraka ya maendeleo ya ghafra na kwa muda mfupi, hivyo kushindwa kuendana sambamba na mifumo
mbalimbali ya kimaendeleo inayotolewa na serikali pamoja na wadau wengine.Vilevile
baadhi ya vikundi kushindwa kushiriki katika vikundi vya kuweka na kukopa
pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha.
Vikundi vingi vya vijana pia vimekosa taarifa juu
ya mifuko rasmi ya vijana ambayo ingeweza kusaidia kuwa chanzo cha fedha
kutunisha mifuko yao na hatimaye kuongeza mitaji waliyonayo, lakini pia hata wakizijua fursa hizo bado kuna
milolongo na vikwazo vingi vya kuwawezesha kupata fursa hizo. Lakini pia vikundi vingi vimekosa elimu ya namna
ya kusimamia shughuli za vikundi na hivyo kupelekea kupoteza dira ya maendeleo.
Angalizo,vikundi vingi vya vijana vinavyojishughulisha na ujasiriamali
huwa ni vikundi vya mazoea, huundwa
kulingana na undugu wa watu Fulani, urafiki
Fulani na hivyo kupelekea mambo mengi kufanyika kwa mazoea. Lakini pia vikundi vingi vya vijana vya
ujasiriamali vinaanzishwa kwa lengo kuu la kupata pesa au kuwezeshwa na mtu
Fulani, na pale msaada unaposhindikana basi hufa mara moja. Hivyo basi ni vyema vijana tunapoamua kuwa pamoja, tunapoamua kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ni
vyema tukaepuka mambo haya, ni bora
mkawa wachache wenye lengo la kujikwamua kiuchumi kuliko kuwa wengi ambao hamna
faida yoyote.
Comments
Post a Comment