YOUTH POTENTIALS FOR COMMUNITY DEVELOPMENT (YOPOCODE)

Youth Potentials for Community development YOPOCODE

Shirika letu limesajiliwa chini ya sheria ya taasisi zisizokuwa za kiserikali kifungu cha 24 ya mwaka 2002.

Shirika letu linafanya kazi nchi nzima isipokuwa visiwani Zanzibar.

Dira yetu ni kuwa shirika kubwa Tanzania litakalo wawezesha vijana kujitambua kwa kutumia uwezo walionao au vipaji au taaluma au rasilimali zinazo wazunguka ili kujiletea maendeleo katika jamii.

1. Ni kutoa elimu itakayowajengea uwezo vijana Tanzania kutambua na kutumia fursa zilizopo katika Jamii zao kwa maendeleo yao na jamii yao.
2. Kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya ujasiriamali na uchumi kwa vijana Tanzania.
3.kuwahamasisha vijana Tanzania kushiriki katika shughuli za maendeleo
4. Kutoa elimu ya uzazi na maambukizi ya ukimwi kwa vijana Tanzania.
5. Kuwachochea vijana Tanzania kushiriki na kukubali mabadiliko ya kisera na kushiriki katika utekelezaji kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Jamii zao na taifa kwa ujumla Wake.

Shirika linawakaribisha watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na wenye akili timamu kuwa wanachama wa shirika letu la youth potentials for community development (YOPOCODE)

Kuna aina Tatu za uwanachama katika shirika letu la YOPOCODE;
A) Wanachama waanzilishi
B) Wanachama wa kawaida
C) Wanachama wadhamini, washauri au walezi.
D) mabalozi wawakirishi wa YOPOCODE Tanzania.

A) Kuomba na kupata ripoti za matumizi ya fedha na maendeleo ya shirika kwa mwaka.
B) kuhudhuria vikao Vyote vya shirika vilevilivyokubalika.
C) kupewa kadi ya uwanachama na nakala ya katiba Mara baada ya kulipa ada ya mwaka ya uwanachama.

A) Kuhudhuria kikao cha wanachama wote cha mwaka
B) Kulipa ada ya mwanachama na michango mwingine itakayopendekezwa na kikao kikuu cha mwaka cha wanachama wote.
C) kujitolea kufanya kazi kulingana na malengo ya shirika.

Comments
Post a Comment