Skip to main content

Posts

YOPOCODE TANZANIA

MAKALA HII MAALUMU KUHUSU UGONJWA HUU WA LUPUS.

MAKALA HII MAALUMU KUHUSU UGONJWA HUU WA LUPUS. MWANDAAJI NA MWANDISHI NI LOOKMAN ADAM LUPUS NI NINI? Huu ni ugonjwa ambao hutokea pale ambapo seli hai zinapogeuka na kuanza kuushambulia mwili..Kazi kubwa ya seli ni kulinda mwili hasa kupambana na magonjwa..ila kwa Lupus seli hizi huanza kuushambulia mwili zenyewe... Zipo dalili nyingi za LUPUS ila hizi ni zile ambazo hujitokeza karibu kwa wagonjwa wengi WA LUPUS 🔹 Uchovu 🔹Maumivu ya Misuli wakati mwingine viungo kushindwa kufanya Kazi 🔹Kifuwa kuwaka moto hasa wakati wa kupumua 🔹Midomo kukauka 🔹Ngozi kutoka vipele vyekundu 🔹Kunyonyoka nywele 🔹Mkojo kutoka ukiwa na damu 🔹Kutoka vipele usoni kama vijipu vidogo 🔹Kupungua uzito 🔹Kukosa hamu ya kula 🔹Kuwa na hasira(Mara chache hutokea) Wakati mwingine LUPUS hufahamika kama SLE (SYSTEMIC LUPUS ERYTHIMATOSUS) Kama nilivyo eleza awalu kuwa LUPUS hutokea pale tu ambapo seli hai zinapogeuka na kuanza kushambulia mwili zenyewe hii hufahamika kama AUTOIMMUNE DISEAS...
Recent posts

SAJILI NGO YAKO TANZANIA

SAJILI NGO YAKO TANZANIA Je, unahitaji ‘NGO’? Fahamu utaratibu wa kusajili NGO ni kifupi cha neno Non-Governmental Organization. Kwa Kiswahili neno hili humaanisha shirika lisilo la kiserikali. Kawaida Serikali huwa ina mashirika yake, kwa mfano Shirika  la Bima, Shirika la  Nyumba, Shirika  la Umeme, mashirika ya vyakula n.k.   Tunapozungumzia NGO maana yake ni kuwa ni mashirika ambayo kwa namna yoyote ile Serikali haihusiki na umiliki wake. Ni mashirika ambayo humilikiwa na watu binafsi.  Serikali huweza kushirikiana nayo tu, lakini si kuyamiliki. Taratibu za uanzishaji, usajili na uendeshaji huratibiwa bayana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002. 1. YAPI YAWE MALENGO YA KUANZISHA NGO Malengo makuu ya kuanzisha NGO yawe ni kusaidia makundi au kundi maalum katika jamii. NGO siyo shirika la biashara.  Siyo kampuni ambayo muanzishaji  wake hutarajia kutengeneza faida. NGO ni shirika la hisani. Ni shirika la kuj...

MARIAM KILYENYI

Tunapozungumzia waambaji wa nyimbo za injili wanaofanya vizuri sana Tanzania, tusisahau huyu Binti yetu @Mariam Kilyenyi ANAENDA KUFANYA UZINDUZI MKUBWA WA ALBAMU YAKE 02/12/2018 KKKT SINZA KUMEKUCHA #Malkiawamoyowaupendo #mamawahaki #BintiAmkaTanzania #Dirayakijanatanzania @MariamKilyenyi https://www.instagram.com/p/BqHqvUagooy/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=i5c6b2btxpc1

ENDELEA KULIPA GHARAMA ZA KUTIMIZA NDOTO ZAKO

ENDELEA KULIPA GHARAMA ZA KUTIMIZA NDOTO ZAKO Kila ukitazama ndoto ambazo umetimiza ni jambo gani linakujia katika tafakari yako? Najua yapo mambo mengi ambayo unakumbuka, jinsi ulivyopambana kuhakikisha unapata hicho ulichokipata. Kuna gharama ulilipa na kwa baadhi ya watu walikuona kana kwamba unacheza. Ndivyo ilivyo, unapojua kile unachokitaka usisubiri watu waseme kuwa ni wazo zuri bali wewe jiamini kuwa hiki ninachokifanya ni sahihi na nitapata matokeo chanya. Jambo lolote zuri kwenye maisha hupatikana kwa kupambana zaidi. Najua Januari 2018 ulijipangia malengo ya kutekeleza mwaka huu. Lakini kila ukiangalia kwenye daftari lako huoni chochote ambacho umefanya au umepambana lakini hakuna matokeo uliyotarajia kupata. Unapoona kuwa hujatimiza malengo yako, ni nini unafanya? Unakata tamaa? Hapana ni kujifunza tu mahali ulipokosea ili kuandika historia mpya kwenye maisha yako. 1. Usiichoke safari ya maisha yako 2. Endelea kujifunza kwani hakuna jambo linaloshindikana 3....

THAMANI YA CHANGAMOTO.

THAMANI YA CHANGAMOTO. NGUVU YA HISIA . Series 05. Saul Kalivubha. Hisia ni sehemu ya binadamu aliye kamili , na hisia ni sehemu ya AFYA , ...lakini kuna NGUVU YA AJABU SANA iliyomo ndani ya HISIA , nayo ni UWEZO WA KUFANYA UPOFU .  Unapoanza kusukumwa na HISIA ,utafanya maamuzi , mwisho wa siku maamuzi hayo yataleta MATOKEO ,....NGUVU iliyomo ndani ya HISIA NI KUKUFANYA KIPOFU , USIONE ATHARI ZA MATOKEO zitakazotokana na MAAMUZI YA HISIA. Hali hiyo ndio inafanya watu wengi wajutuie maamuzi ya HISIA  waliyoyafanya huku wakiamini ni sahihi kwa wakati ule ,lakini leo wanaishi MATOKEO yanayowaumiza. TIBA: HISIA hushawishi MAAMUZI, jitahidi  sana ufahamu athari za maamuzi kabla na HISIA isiwe ndio sababu ya kwanza KUKUFANYA UAMUE . http://kalivubha.blogspot.com/2018/02/mambo-matano-muhimu-kabla-ya-biashara.html?m=1 Facebook na instagram , tembelea kurasa zetu za FIKIA NDOTO ZAKO.      FIKIA NDOTO ZAKO.        0652 1237...

HOW TO BE A COMEDY WRITER

JAMII 100; Vichekesho na Ucheshi katika sura ya biashara ya kale iloanza kukua toka zamani na itazidi kukua kadri muda uendavyo. Mambo ya kuzingatia; Vichekesho ni fursa kubwa kibiashara na imetengeneza wafuasi wengi kwa maana kucheka ni moja ya tiba na kuipa akili utulivu. Kitabu; HOW TO BE A COMEDY WRITER, Secrets from the inside by Marc Blake ( Namna ya kuwa mwandishi wa vichekesho, siri kutoka ndani ) Vitimbi, Mizengwe, Futuhi, Joti Tv, Ze komedi, Cheka tu, Churchill show, Omondi, Mc Pilipili ni moja ya picha kubwa kwa namna gani vichekesho au ucheshi ulivyofanya maisha ya watu wengi wapende kufuatilia na kufurahi wasikiapo au wakitazama. Kucheka kuna raha yake na tunaona namna hata mwili huwa katika utulivu pale ambapo unakutana na kitu cha kukufanya ucheke. Je umewahi jiuliza kwanini watu hucheka ?, nini kinachowasukuma watu walipe na hata kuhudhuria majukwaa ya ucheshi. Inawezakana ikawa ni zoezi gumu kuelezea kwa maneno lakini ucheshi au vichekesho vinakufanya ujisikie vi...

HII PIA NI SABABU

HII PIA NI SABABU Yapo mambo mengi yanayosababisha ndoto kutotimia kwa watu wengi. Lakini hii ya kutokujua unataka nini hasa ndiyo sababu inayopelekea watu wengi kufanya vitu vingi na kuviacha havijatimia. Tunapokaribia mwishoni mwaka, kipindi cha tathimini binafsi ya mwaka mzima unajikuta huna ulichotimiza ila una mengi ambayo januari mpaka novemba umeacha na kuishia njiani. Kujua nini unataka katika safari ya maisha yako utapelekea kupigania nakuhakikisha unatimiza adhima hiyo. Watu wengi hawajui nini wanataka hivyo hata wanapojiwekea malengo yao bado hawanauhakika kama ni kweli ndicho wanachokitaka. Mwanajeshi anapokosa shabaha vitani na kumimi tu risasi sehemu ambayo adui hayupo, humaliza risasi zake na huwa katika hatari ya kipigwa na adui. Nini tunajifunza hapa::: 1. Jua unataka nini kwenye maisha haya unayoishi 2. Chukua kitu kimoja kifanye kwa muda mrefu mpaka pale utakapo pata matokeo chanya. Endelea kung'ang'ania usiwe mwepesi kukata tamaa. 3. Pasipo maono ...