Binti Amka Tanzania, ni kampeni
inayoratibiwa na viongozi wa YOPOCODE kwa Kushirikiana na MABALOZI WA BINTI
AMKA TANZANIA. Kampeni hii inalenga kumsaidia mtoto wa kike Tanzania kufikia
malengo yake kielimu, kiuchumi na kiuongozi/kisiasa, inalenga kupambana na
changamoto mbalimbali zinazomkwamisha mtoto wa kike kufikia ndoto zake ikiwemo
ndoa na mimba za utotoni, utoro wa masomo, mfumo dume katika jamii, kukosekana
mahitaji na mifumo sawa kwa jinsia zote kupata fursa sawa na vipaumbele sawa.
kwa
mjibu wa shirika la watoto duniani UNICEF kumekuwa na ongezeko kubwa la mimba
mashuleni kutoka 23% hadi 26% yaani takribani watoto 8000 hapa Tanzania kila
mwaka hukatisha masomo kwa ajili ya ujauzito na ndoa za utotoni ambazo kwa
kiasi kikubwa huathiri ndoto zao za kielimu, kiuchumi na kisiasa.
Vilevile idadi kubwa ya watoto wa kike
wamekuwa wakimaliza elimu ya msingi lakini upoteza nafasi ya kujiendeleza
kielimu hata pale wanapokuwa wamechaguliwa kujiunga na sekondari nayo imekuwa
ikiongezeka, pia kushuhudia kuongezeka kwa vitendo vya kikatili wa kingono kama
ubakaji na ulawiti kwa watoto wakike na chakusikitisha zaidi vitendio hivyo
vimekuwa vikifanywa na ndugu wa karibu sana wa watoto hawa wakiwemo
wazazi,walezi, majirani na hata walimu uko mashuleni matukio haya yamekuwa
hayaripotiwi kwenye vyombo vya sheria kwani mengi huzungumzwa kifamilia na
kuwaacha watuhumiwa wakiendelea na maisha yao..
Inasikitisha kuona kuwa mtoto wa kike hapa
nchini bado wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi na cha kusikitisha zaidi
mtoto huyu anaanza kubaguliwa kuanzia katika ngazi ya familia.Katika familia
nyingi za kitanzania mtoto wa kike amekuwa akikosa fursa ya kupata Elimu
ukilinganisha na mtoto wa kiume na katika mazingira mengine wazazi wamediriki
hata kuwaozesha watoto wao wa kike kwa ajili ya kupata fedha ya kusomesha
watoto wa kiume. Ukiangalia pia katika suala zima la Elimu ni ukweli
usiofichika kuwa idadi ya wasichana wanaoshindwa kumaliza masomo kwa sababu za
kupata mimba imekuwa ikiongezeka.
MAJUKUMU YA “MABALOZI WA BINTI AMKA TANZANIA”
1. Kuhakikasha
upatikanaji wa taarifa sahihi za mabadiliko yanayotokea katika mwili wa mtoto
wa kike pindi anapovunja ungo.
2.
Kutoa elimu ya kujitambua kupitia semina, makongamano na clubs mbalimbali zenye
lengo la kumsaidia mtoto wa kike kufikia malengo yake kielimu, kiuchumi na
kiuongozi
3.
kuwawezesha MABINTI kwa kuwajengea uwezo
Wa kujitambua na kutumia rasilimali zinazo wazunguka na fursa mbalimbali
zinazopatikana katika maeneo yao kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii.
4.
Kuwahamasisha vijana wa kike kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuwa
sehemu ya mabadiliko na kujikwamua kiuchumi na kuondoa dhana tegemezi.
TANZANIA BILA MIMBA NA NDOA
ZA UTOTONI INAWEZEKANA
TUSHIRIKI KATIKA KAMPENI YA
BINTI AMKA TANZANIA KUMSAIDIA MTOTO WA KIKE KUFIKA MALENGO YAKE KIELIMU,
KIUCHUMI NA KIUONGOZI
KARIBU UWE BALOZI WA KAMPENI
YA BINTI AMKA TANZANIA “JIUNGE KWA WHATSAPP NO 0758051641
Comments
Post a Comment