DIRA YA KIJANA TANZANIA
BY ALFRED MWAHALENDE
2017
Yaliyomo
I kijana ni nani?
2 ujana ni nini?
3 sifa na wajibu wa kijana
4 nafasi ya kijana katika maendeleo ya jamii
5 vijana kushiriki katika maendeleo ( fursa
zilizopo Tanzania vijana kujiwekeza)
6 je, kijana ni taifa la leo au kesho?
7 mifano na historia ya vijana/vijana waliowahi
kufanya vizuri
8 biashara, ujasiriamali na makundi ya
ujasiriamali kwa vijana
9 changamoto zinzowakwamisha vijana katika kufikia
ndoto zao
10 mipango na mikakati ya Tanzania mpya ya vijana.
Kijana ni nani?
Ø
Neno kijana linatafsiriwa katika tafsiri
tofauti katika kila jamii, Mathalan nchini Tanzania kijana ni mtu mwenye umri
wa kati ya miaka 18 hadi 35, yaani baada ya balehe. Mabadiliko makubwa ya
kimaumbile hutokea sambamba na kukomaa kwa mawazo.
Ø
Aidha Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya Maendeleo ya
Vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, kijana ni mtu mwenye
umri kuanzia miaka 15 hadi 24.
Ø
Hali kadhalika Kwa tafsiri ya umoja wa
mataifa, Kijana ni mwanamke au mwanamme aliye na umri kati ya miaka 15 hadi 24.
Tafsiri hii hutofatiana kutoka nchi moja hadi nchi nyingine. Nchi au maeneo
mengine ya dunia huwa na tafsiri tofauti kulingana na mahitaji ya mazingira na
maeneo yao, na pengine kwa mujibu wa mifumo ya kijamii,kisiasa na kisheria
katika nchi hizo.
Ø
Katika mikataba na sheria mbalimbali za kimataifa zinafafanua kuwa
binadamu mwenye umri kuanzia miaka 0-17 ni mtoto na haruhusiwi kufanya maamuzi
yeyote mazito kuhusu maisha yake, ingawa kamusi tajwa hapo mwanzo inaleta utata
katika vipande viwili vya umri hasa katika maana ya kijana,kamusi inasema
kijana ni mwana mdogo,mtoto mwenye umri wa miaka 7 hadi12.
Ø
Lakini katika mtazamo wa
kawaida tunaamini kuwa kijana ni binadamu mwenye umri wa
Ø
Kuanzia miaka 18-40 na wakati mwingine mpaka miaka 45.
Comments
Post a Comment