Skip to main content

Posts

KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA YAANZA RASIMI JIJINI DAR ES SALAAM.

KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA YAANZA RASIMI JIJINI DAR ES SALAAM. ☑ Yopocode kwa kushirikina na Mabalozi wa kampeni ya Binti Amka Tanzania wameanza rasimi kampeni katika shule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam. ☑ Akizungumza kwa niaba ya shirika la vijana Tanzania la YOPOCODE, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Alfred Sostern Mwahalende amekuwa na haya ya kusema"kampeni ya Binti Amka Tanzania inalenga kumsaidia mtoto wa kike nchini  kufika ndoto yake na malengo yake kielimu, kiuchumi na kiuongozi na katika hili pia tutalenga kupambana na masuala ya mimba na ndoa za utotoni ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakichangia katika kumkwamisha mtoto wa kike kufikia malengo  yake.Tumeanza na shule za misingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam huku tukifanya juhudi katika halmashauri zingine na mikoa mingine ambayo tayari tumeanza maandalizi ya kuzindua kampeni yetu" Katika kuhakikisha tunafikia lengo la...

Binti Amka Tanzania

YOPOCODE kwa kushirikikiana na Mabalozi Wa Kampeni Ya Binti Amka Tanzania kanda ya/Dar es salaam na Pwani wanafanya kampeni mahususi inayolenga kumsaidia mtoto wa kike kufikia malengo yake kielimu, kiuchumi na kiuongozi. Aidha kampeni inalenga kupambana na changamoto mbalimbali zinazomkwamisha mtoto wa kike kufikia ndoto zake ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, utoro wa masomo, mfumo dume katika jamii, kukosekana mahitaji na mifumo sawa kwa jinsia zote, kupata fursa sawa na vipaumbele sawa. Tumependekeza maeneo mbalimbali kuyafikia ikiwemo shule za misingi na sekondari ili kufanikisha kampeni yetu ya Binti Amka Tanzania. Binti Amka Tanzania Alfred Mwahalende Alfred Mwahalende YOPOCODE TANZANIA Youth Potentials for Community Development - Yopocode Yopocode-Singida Youth Potentials For Community Development